Kurasa

Friday, April 27, 2012

UTAJIRI WA WAZIRI MAIGE WAPINGWA KILA KONA

Nyumba ya mweshimiwa Maige.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige 
SIKU moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige kukiri kununua nyumba jijini Dar es Salaam kwa Dola za Marekani 410,000, taasisi na watu mbalimbali wameeleza kutoridhishwa na utajiri wake, huku Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) likitaka ashtakiwe kwa kuhujumu uchumi.
Kiukweli imekua gumzo kwa kiasi kikubwa kwa watanzania waziri kumiliki nyumba ya dhamani kiasi hiki wakati watanzania wafa njaa.
wengi wanahoji maswali kama haya;
“Hivi inawezekana kweli kipaumbele cha kwanza cha mbunge huyo kijana iwe ni nyumba ya thamani kubwa kiasi hicho? Na kama ndio kipaumbele chake ina maana ana utajiri wa kiasi gani na ameupata vipi?”  "Hivi ni vitu vingapi anamiliki ambavyo thamani yake hatujui?”
Mh. Ezekiel Maige

GAZETI LETU LEO.


Thursday, April 26, 2012

GAZETI LA LEO


UNAJUA HIKI KUHUSU MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR


Mwalimu.

Hii leo 26 April tukiwa tunaadhimisha miaka 48 ya muungano, Je, unalifahamu hili juu ya muungano.
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar. 
     Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
    Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika,  kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.
     Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.
     Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
      Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
      Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil.
     Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano ambayo ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
      Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.
      Katiba hiyo ilianisha serikali mbili, uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande  wa Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
       Hata hivyo mambo ya Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya Muungano.
       Mwaka 1985, jambo la 12 linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.
     Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.
     Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki.
     Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.

Wednesday, April 11, 2012

Mojawapo ya tsunami huko nchini Thailand.


GAZETI LA LEO


Mr. Kanumba
Nyimbo iliyoimbwa na Marehemu Kanumba inaitwa "NITAINUA MACHO YANGU JUU"....Moja ya mistari kwenye hii nyimbo ni ""Kama leo nikifa kila mtu atanisifu kwa lake ******* ,ata hao wanaonichukia watabeba jeneza langu kwa nyimbo na sala za uzuni,Mwenzangu leo niko hai twachukiana sana , usoni wa cheka rohoni ni vita,Tusameane tuishi kwa upendo na amani,Furaha yetu hadi mbinguni tuwe na furaha ya… 'sema na moyo wangu eee baba'

KANUMBA KAZIKWA

Hekima yake, Busara yake, Ucheshi wake, Uadilifu wake daima iwe funzo kwetu vijana. Pumuzika kwa amani Steven Kanumba.

Monday, April 9, 2012

Hizi ni baadhi ya Picha za Seteven Kanumba, Kipindi cha Uhai wake.







Ki ukweli katutoka Steven Kanumba.

Ni ngumu kuamini ni kama kalala, kama ataamuka , lakini hatinaye tenda kipenzi wetu kwa rika zote. wototo walizoea kumwita Uncle JJ kila ukipita mitaana lakini kiukweli uwepo wake umetoweka hatunaye tena dunia. Japo kila mwenye uhai lazima aonje mauti unaweza kujiuliza kwanini iwe hivi katika umri mdogo kiasi hiki kijana mwenzetu kututoka kakini hatuna la kupinga lililo pangwa na Mungu ni vigumu mwanadamu kulipangua.
Mr. Kanumba
Katutoka ndugu yetu kipenzi Mr Kanumba tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi jina la Bwana lihimidiwe Amen.

Kutoka mwananchi " Mama mzazi wa marehemu Stevin Kanumba, Flora Mutegoa amekubali mwanae azikwe kesho tarehe 10 / 4/ 2012 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa10 jioni."