Kurasa

Friday, April 27, 2012

UTAJIRI WA WAZIRI MAIGE WAPINGWA KILA KONA

Nyumba ya mweshimiwa Maige.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige 
SIKU moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige kukiri kununua nyumba jijini Dar es Salaam kwa Dola za Marekani 410,000, taasisi na watu mbalimbali wameeleza kutoridhishwa na utajiri wake, huku Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) likitaka ashtakiwe kwa kuhujumu uchumi.
Kiukweli imekua gumzo kwa kiasi kikubwa kwa watanzania waziri kumiliki nyumba ya dhamani kiasi hiki wakati watanzania wafa njaa.
wengi wanahoji maswali kama haya;
“Hivi inawezekana kweli kipaumbele cha kwanza cha mbunge huyo kijana iwe ni nyumba ya thamani kubwa kiasi hicho? Na kama ndio kipaumbele chake ina maana ana utajiri wa kiasi gani na ameupata vipi?”  "Hivi ni vitu vingapi anamiliki ambavyo thamani yake hatujui?”
Mh. Ezekiel Maige

No comments:

Post a Comment