Kurasa

Monday, February 11, 2013

Papa Benedict XVI atangaza kujiuzuru.



Habari kutoka Vatican zinasema kuwa, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI atajiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa Februari mwaka huu.
Taarifa kutoka ofisi ya Papa imesema kuwa, hatua hiyo imetokana na kuendelea kudhoofika afya ya kiongozi huyo wa kidini. Papa Benedict XVI mwenye umri wa miaka 85 alichaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki Aprili 19 mwaka 2005 baada ya kufariki dunia Papa John Paul II.
Papa Benedict XVI anakuwa kiongozi wa pili wa kanisa katoliki kujiuzulu. Mwaka 1296, Celestine V alijiuzulu kutokana na sababu za kiafya.

No comments:

Post a Comment